Habari,
Natumaini unaendelea vizuri. Leo nimejaribu kutumia laughable adhimu ya Kiswahili kuelezea historia ya watoto wa Fatima. Kwa wakatoliki wanajua hii hadithi vizuri zaidi.
Hii Nyimbo inaendana na hadithi.
Ilikuwa ni tarehe 13/10/1917 muda wa saa saba na nusu hivi za mchana, wakazi wa mji wa Fatima huko Portugal walikuwa wamekusanyika katika eneo linaloitwa Cova Da Iria, nje kidogo ya mji wa Fatima.
Maelfu kwa maelfu ya wakazi hao walisimama mbele ya Lucia, Jacinta na Francisco
Kilikuwa ni kipindi cha mvua na manyunyu na anga lote lilikuwa limefunikwa na mawingu na ukungu kila mahali.
Ardhi ilikuwa imeloana sana na kila mahali kuliwa na matope na madimbwi ya maji.
Mara ghafla kikatokea kitu kama nguzo ya moshi yenye rangi ya bluu iliyokolea sana na kung’aa, na kusimama juu ya vichwa vya Lucia, Jacinta na Francisco.
Nguzo hiyo nyembamba sana ilikuwa na urefu kama mita mbili hivi kwenda juu na baada ya sekunde kadhaa ikapotea.
Mara ghafla tena nguzo hii ikatokea tena mara ya pili na mara ya tatu na kisha ikatoweka.
Watu wakiwa bado wanaishangaa nguzo hii iliyokuwa na mwangaza wa ajabu, mara nikasikia kelele za watu kutoka nyuma yangu, nilipogeuka nikaona watu wote wanatazama juu angani.
Kufumba na kufumbua, mawingu yakaanza kutoweka na mwanga mkali wa jua ukachomoza, ardhi yote ikakauka mara ile na ikawa kama vile mvua haijanyesha kabisa.
Cha ajabu jua hili lilikuwa halichomi wala haliunguzi, wala haliumizi macho licha ya watu kutizama juu!
Ghafla jua likabadilika na kuwa kama vile limepatwa (Solar Eclipes), likawa linaonekana kama pete yenye kung’aa sana na mwangaza wa dhambarau ukaijanza nchi yote! Vitu vyote pamoja na watu na miti, wakawa kama rangi ya dhambaru.
Eneo lote likawa na mwanga wa dhambarau wenye kupendeza na kustaajabisha!
Nikasikia tena kelele za watu kwa nguvu sana, na sasa jua likawa linacheza cheza angani kama vile balbu inayoning’inia, likawa kama vile linataka kudondoka, nikasikia ndani yangu hisia fulani hivi mbaya sana ambayo siwezi kuilezea kabisa.
Kelele za watu zikazidi mno, huku wengine wakipiga magoti na kusali. Baada ya sekunde chache ile hali ikatoweka na jua likarudi katika hali yake ya kawaida.
Anaelezea Dr. Jose Maria de Almeida Garrett, Professor wa kitivo cha Sayansi katika chuo cha Coimbra Portugal, ambaye alishuhudia kwa macho yake na kuandika kwa mikono yake.
Katika maisha yangu sikupata kuona jua likiwa hivi, nimeshuhudia kupatwa kwa jua lakini siyo kama hivi, hili lilikuwa ni tukio la ajabu sana.
Tukio hili wengi walilipa jina “The miracle of the Sun”(miujiza ya jua). Maandishi haya yanapatikana kwenye kitabu kiitwacho “Novo Documentos de Fatima” kilichoandikwa na Professor huyu mwaka 1922.
Kabla ya tukio hili la “miujiza ya jua” kutokea, watoto Lucia, Francisco na Jacinta walikuwa wamewajulisha wakazi wa mji wa Fatima kuwa tukio hilo litatokea siku hiyo na ndiyo maana wakazi wote walikusanyika ili kushuhudia.
Watoto hawa walisema waliambiwa na “Mwanamke wa Ajabu” aliyewatokea kabla, na kusema ili wakazi wa Fatima waamini maneno yake, basi wajikusanye hapa Cova Da Iria kuja kushuhudia muujiza atakaoufanya.
Mwanamke huyu wa ajabu ambaye alikuwa akiwatokea watoto hawa watatu mara moja kwa mwezi kwa miezi sita mfululizo, wengi waliamini au kuaminishwa na Kanisa Katoliki kuwa yeye ni Bikira Maria (mama wa Yesu).
Kati ya hawa watoto watatu ni mmoja tu,Lucia, ndiye aliyekuwa anazungumza na Mwanamke huyu na wengine, Jacinta na Francisco walikuwa wanamwona tu bila kusikia nini anaongea, hayo yalisemwa na Lucia wakati wakihojiwa na Priest wa mji huo wa Fatima, Priest Manuel Marques Ferreira.
NI NINI HASA KILITOKEA?
Mara ya kwanza kabisa watoto hawa watatu kutokewa na kitu wasichoweza kukitambua ilikuwa ni mwaka 1915, wanasema waliona kitu angani, hawakutambua ni kitu gani.
Watoto hawa ni Lucia Dos Santos aliyekuwa na miaka 8, Jacinta Marto miaka 5 na Francisco Marto miaka 7.
Mwaka uliofuatia yaani 1916 wakasikia sauti ikiwapa ujumbe, ikiwaambia kuwa kuna jambo litatokea.
Ilipofika tarehe 13/05/1917 wakiwa eneo la Cova da Iria chini ya mti wa Mwaloni (Oak Tree), mara wakamwona mwanamke wa ajabu akiwatokea.
Mwanamke huyu alikuwa amesimama akielea angani bila kukanyaga chini.
Kwa mujibu wa Lucia ambaye ndiye alikuwa mkubwa kati ya hao watoto akiwa na miaka 10 kipindi hicho, anasema, Mwanamke huyu alikuwa amevaa mavazi meupe yanayotoa mwangaza wa ajabu.
Kuanzia kichwani alikuwa amejifunika mtandio na mtandio huo ulikuwa kwa nyuma mgongoni unafika mpaka chini.
Alikuwa amevaa kitu kama koti jeupe na blausi nyeupe na sketi fupi sana iliyoacha mapaja yake kwa mbele wazi! Kiunoni alikuwa amefunga mshipi au mkanda wa dhahabu.
Macho yake yalikuwa meusi sana, tofauti kabisa na macho ya binadamu yalivyo. Huwezi kutofautisha kati ya jicho na mboni ya jicho, lote lilikuwa jeusi, alikuwa anatisha.
Shingoni alikuwa amevaa mkufu wa dhahabu safi inayong’aa, ikiwa na kidani kikubwa cha mviringo kama pete kubwa au Medallion.
Mkono wake wa kulia alikuwa ameshika kitu kama mpira au tufe hivi likiwa na rangi ya rubi. Miguuni hakuwa amevaa viatu bali alikuwa amevaa soksi ndevu nyeupe sana zilizoishia karibu na magoti.
Lucia anaendelea kusema, tukaogopa sana, nikamuuliza wewe jina lako ni nani? Akajibu kwa kunyoosha kidole chake juu na kusema; “I am a Lady”, yaani mimi ni Mwanamke.
Hapa tunaona kwamba mwanamke huyu hakusema kuwa yeye ni Bikira Maria mama wa Yesu, bali alisema I am a Lady! Je kama ni kweli alikuwa Bikira Maria, angevaa nguo inayoacha mapaja yake wazi?
Lucia anasema kwamba Mwanamke huyu akaongea naye mambo mengi na kumpatia maagizo mengi sana ili ayafikishe kwa Kanisa Katoliki.
Maelezo aliyopewa akaambiwa mengine ni siri kubwa na hatakiwi kumwambia mtu yeyote mpaka atakapopewa maagizo na yeye mwenyewe.
Siri hizo Lucia aliziweka katika mafungu matatu. Tena ikumbukwe kuwa kati ya hawa watoto aliyekuwa anamsikia na kuongea na huyu Mwanamke ni Lucia peke yake, wengine Jacinta na Francisco walikuwa wanamwona tu pasipo kusikia maongezi yoyote!
Mwanamke huyu wa ajabu akamwambia Lucia kuwa atakuwa anakutana nao mara moja kwa mwezi kwa muda wa miezi sita mfululizo yaani kuanzia mwezi huo wa tano mpaka mwezi wa kumi.
Kila mwisho wa mwezi wakutane nae hapo ili awape maagizo zaidi. Na ikifika mwezi wa kumi tarehe 17 wawalete watu wote wa mji wa Fatima mahali hapo ili awaoneshe muujiza.
Lucia anasema kwamba Mwanamke huyu wa Ajabu aliwaonesha maono jinsi watu wenye dhambi na shetani watakavyotupwa kwenye ziwa la moto.
Tena akamwambia Lucia kuwa Jacinta na Francisco watakufa wakiwa bado wadogo sana, kwani atawachukua na kuwapeleka mbinguni.
Sasa wengi sana wanajiuliza, Je! Mwanamke huyu wa ajabu ni kweli alikuwa ndiye Bikira Maria Mama wa Yesu?
Ili tupate jibu la huyu mwanamke ni nani hebu tusome kile alichokisema maana kwa maneno yake mwenyewe aliyotamka tutajua yeye ni nani.
–Akanyoosha kidole chake juu mbinguni na kusema; “I am a Lady” akimaanisha mimi ni mwanamke.
Wengine wanasema vile kunyoosha kidole chake juu alimaanisha..”I am the Lady of Heaven” yaani mimi ni Mwanamke wa mbinguni au “mama wa mbinguni”.
Lakini hakusema yeye ni Bikira Maria. Ukisoma kitabu cha Isaya, Yeremia na Ufunuoa utaona nini MUNGU ameahidi kumfanya huyu “Malkia wa Mbinguni”.
–Akamwambia Lucia; “waambie wanijengee mahali hapa kanisa kwa ajili ya moyo wangu safi na utukufu wangu.
–Akamwambia Lucia, waagize wasali Rosari kila wakati na kuvaa Brown Scapular maana wakifanya hivyo wataokolewa katika dhambi.
–Akamwambia Lucia, “waagize waniamini mimi maana ni mimi peke yangu kwa uwezo wa moyo wangu safi (Immaculate heart) ninao uwezo wa kuwaokoa katika dhambi zao na kuwafikisha mbinguni.
–Akamwambia Lucia, “kawaambie kwamba Mungu amekusudia kuanzisha dunia Ibada kwa ajili ya moyo wangu safi”. Yaani wanadamu wakifanya Ibada wafanye pia Ibada kwa ajili ya moyo safi wa Mwanamke huyu na hayo ni maagizo ya Mungu.
Mwezi wa 11 mwaka 2001 wakati Lucia akihojiwa, akaweka msisitizo kuwa ni kweli kabisa kuwa Ibada zikifanyika kwa ajili ya Moyo Safi wa Maria, uwokovu utakuja juu ya Kanisa na kwa wanadamu wote.
Anyways, Mwanamke huyu wa Ajabu alimwagiza Lucia mambo mengi sana ambayo siwezi kuyaandika yote maana nikiandika yote huu uzi utakuwa mrefu sana.
Baadhi ya maneno aliyomwambia Lucia ni pamoja na kutabiri vifo vya Jacinta na Francisco ambapo alisema watakufa wakiwa bado wadogo, na yeye Lucia akaambiwa ataishi maisha marefu.
Francisco Marto alikufa mwaka 1919 tarehe 4 mwezi wa 4, akiwa na umri wa miaka 11 tu! Aliugua na kufa. Ikumbukwe kuwa Francisco wakati wanatokewa na huyu “Mwanamke wa Ajabu”, alikuwa na miaka 9 tu, hivyo miaka miwili baadaye akafa!
Jacinta Marto alikufa mwaka 1920 tarehe 20 ya mwezi 2 akiwa na umri wa miaka 9 tu! Naye pia aliugua na kufariki. Wakati wanatokewa Jacinta alikuwa na umri wa miaka 7. Jacinta na Francisco walikuwa mtu na kaka yake na Lucia alikuwa ni binamu yao.
Kuna wakati Lucia alikaririwa akisema kwamba walipotokewa na Mwanamke yule, kutokana na hofu waliamua kuifanya iwe siri yao wao watatu lakini Jacinta hakuweza kutunza siri na akawa wa kwanza kusema mbele za watu hivyo ikambidi Lucia aelezee yote waliyoona na kusikia.
Baada ya wenzake kufa, Lucia aliendelea kusambaza ujumbe na maagizo aliyopewa na yule Mwanamke. Lucia akajiunga na chuo cha Masister na akawa mtawa wa kanisa katoliki.
Lucia ameandika barua nyingi sana kwa kanisa katoliki enzi za uhai wake. Alifariki dunia mwaka 2005 tarehe 13 ya mwezi wa 2 akiwa na umri wa miaka 97.
Katika historia ya kanisa katoliki kumekuwa na matukio ya Apparitions (kutokewa na Mwanamke) mara nyingi sana.
Katika na uzi huu kuwa mrefu nitakuja na uzi mwingine na kuwaandikia hizo zinazoitwa Marian Apparitions zilipotekea na ziliwatokea akina nani na zilisema nini.
Swali la kujiuliza Je ni kweli huyo analiyewatokea akina Lucia, Jacinta na Francisco alikuwa Bikira Maria?
Mimi sikupi jibu, ishughulishe akili yako mwenyewe ili uijue kweli nayo hiyo kweli itakuweka huru kweli kweli.
Furahia hadithi hii.